Kimuna ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Wamuna kwenye visiwa vya Muna, Buton na Ambon. Mwaka wa 2007 idadi ya wasemaji wa Kimuna imehesabiwa kuwa watu 300,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kimuna iko katika kundi la Kicelebiki.